Gabriel Martinelli: ‘Je Man United ilimkosa ‘Cristiano Ronaldo mpya wa Arsenal’?

Gabriel Martinelli: ‘Je Man United ilimkosa ‘Cristiano Ronaldo mpya wa Arsenal’?

Wakati klabu ya Manchester United ilikuwa ikijikakamua kupata sare katika klabu ya AZ Alkamaar katika ligi ya Ulaya, mchezaji waliyemfanyia majaribio alikuwa akifunga magoli mawili katika dakika mbili katika nashindano hayo hayo akiichezea Arsenal.

Kijana Gabriel Martinelli alifunga mabao manne katika mechi mbili akichezea Gunners huku akiisaidia timu yake kuilaza Standard Liege 4-0 siku ya Alhamisi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alikuwa akizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi jioni, ikimwangazia mchezaji huyo mwenye kipaji ambaye anatarajiwa kuwa nyota wa Brazil.

Bila shaka Martinelli ameanza vizuri kazi yake Arsenal, kwa mchezaji aliyegharimu Gunners pauni 6m msimu uliopita baada ya mashabiki wengi kujiuliza yeye ni nani?

Mvulana kutoka Brazil anayepigiwa debe kuwa nyota

Mashabiki wachache walimjua Martinelli wakati aliposainiwa kwanza kujiuga na Arsenal wakati wa dirisha la uhamisho akijjiunga kutoka katika klabu ya Brazil ya Ituano mwezi Julai.

Hatahivyo nyumbani kwao anaonekana kuwa na kipaji cha kumrithi Neymar na tayari ameonyesha kile anachoweza kufanya katika mechi mbili pekee za Arsenal.

Ameichezea klabu hiyo mechi mbili katika ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Nottingham Forest katika kombe la Carabao na siku ya Alhamisi usiku alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya klabu ya Ubelgiji Standard Liege.

Katika mechi zote alizocheza kufikia sasa , Martinelli amevutia wengi kutokana na kasi yake na udhibiti wa mpira.

Kama mchezaji mwenza Phillipe Coutinho, uhodari wake ulinolewa kwa kucheza Futsal akiwa mdogo.

Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Corinthians akiwa na umri wa miaka 9 hadi 14 wakati alipojiunga na timu ya daraja la nne nchini Brazil Ituano 2015.

Martinelli kama vijana wengi , alikuwa akimuenzi nyota wa Portugal Cristinao Ronaldo na anadai kwamba anacheza kama yeye.

Emery amsifu Martinelli
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefurahishwa na kile ambacho Martinelli anaweza kuafikia akiichezea Arsenal, lakini bado hajajisahau.

”Kitu chake cha kwanza kilichopo akilini mwake ni kutusaidia” , alisema baada ya ushindi huo katika kombe la Yuropa.

Wakati wa mechi za maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu , alikuwa mzuri sana kila akicheza.

”Nilizungumza naye na kumuomba kuwa mtulivu kwa sababu wakati fursa yake itakapofika iwapo ataendelea na hamu hiyo ya kutaka kufunga ataendelea vyema”. Kasi yake ni nzuri mno.

”Na mara nyingi hupendelea kucheza wingi ya kulia. Nataka kumtumia kama mshambuliaji kwa kuwa alicheza katika safu hiyo na Brazil”.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha ESPN nchini Brazil mapema mwaka huu, Martinelli alifichua kwamba alifanyiwa majaribio kadhaa na Manchester United katika kipindi cha miaka miwili kutoka 2015.

Kulingana na chombo cha habari cha Manchester Evening News wakati huo mchezaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 14 alicheza pamoja na Mason Greenwood katika mechi ya kirafiki kwa timu ya vijana ya United dhidi ya timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 ya Lincoln.

United ilishinda 2-0 lakini United haikuonyesha hamu tena na mchezaji huyo.

”Kati ya 2015 na 2017, nilienda huko mara nne na kufanya mazoezi nao kwa takriban siku 15”, alisema Martinelli. ”Nilikutana na wachezaji wote wa kulipwa. Niliomba kupigwa picha na Patrice Evra, Marouane Fellaini na wengine.

”Paul Pogba alijua kwamba mimi ni raia wa Brazil na kuniuliza iwapo kila kitu kilikuwa shwari na pale nilipokuwa nikicheza. Tulipiga picha . Klabu ya Ubelgiji ya Gent na pia mbaingwa wa ligi ya Uhispania Barcelona pia walimchunguza mchezaji huyo kabla ya Arsenal kumsajili na kumpeleka Ulaya.

Sio timu hizo pekee

Ni muda pekee utakaosema iwapo Arsenal imempata mchezaji bora aliyetupwa na wapinzani wake na kuamua kumsajili.

Lakini kandanda imezungukwa na hadithi za klabu kuwauza wachezaji kabla ya wachezaji hao kung’ara katika klabu zao mpya na Arsenal pia haikusazwa.

Mwaka 2016 Arsenal ilimuuza Serge Gnabry kwa Werder Bremen kwa dau la £5m.

Mshambuliaji huyo alirudi mjini London mapema wiki hii na Bayern Munich akifunga magoli manne katika ushindi wa 7-2 katika mechi za kombe la klabu bingwa dhidi ya Tottenham.

Mchezaji mwengine wa Arsenal Donyell Malen alifunga mara mbili huku PSV ikiilaza Rosenberg 4-1 katika kombe la Yuropa alhamisi .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alifunga magoli 12 katika mechi nane alizochezea PSV , mbali na kufunga goli lake la kwanza akiichezea timu ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Ujerumani.