Mashabiki wa Club Africain ya Tunisia wachanga dola $450,000 kwa siku moja kuikwamua

Mashabiki wa Club Africain ya Tunisia wachanga dola $450,000 kwa siku moja kuikwamua

Mashabiki wa Club Africain ya Tunisia wamechangishana zaidi ya dola za Marekani 450,000 kwa siku moja kwa ajili ya kuikwamua kiuchumi klabu yao, miongoni mwa wapenzi wake ni mwanaume mmoja ambaye alichagua kuacha dawa ili kuikoa timu yake pendwa.

Club Africain, Timu kongwe ya pili nchini Tunisia na maarufu barani Afrika, imenyang’anywa alama sita na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwa kushindwa kuwalipa mishahara wachezaji wao wa zamani.

Ili kuisaidia klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1920, Shirikisho la soka nchini Tunisia (FTF) iliunda kamati kwa ajili ya kuiokoa timu dhidi ya vikwazo zaidi.

Mwezi Oktoba, FTF walifungua akaunti ya benki ili wapenzi wa timu hiyo wasaidie kulipa madeni ambayo yamefikia dola za kimarekani 600,000 mpaka sasa.

Kwa ujumla na michango ya Jumanne, ambayo ilikusanywa kwa kipindi cha saa 24, inamaanisha klabu hiyo imechangisha zaidi ya dola milioni moja.

Katika Kampeni ya saa 24, watoto walifika na mikebe na mshabiki wa klabu hiyo ambaye ni mlemavu wa macho alipeleka fedha alizokuwa akichanga kwa ajili ya matibabu yake ili kuisaidia timu yake.